Ruka hadi Yaliyomo

(1) Sura hii inahusu Tume zote zilizotajwa katika ibara ya (2) na afisi huru zilizotajwa katika ibara ya (3), isipokuwa pale ambapo imetajwa vinginevyo.

(2) Tume hizo ni–

  • (a) Tume ya Haki za Binadamu na Usawa;
  • (b) Tume ya Kitaifa ya Ardhi;
  • (c) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka;
  • (d) Tume ya Huduma za Bunge;
  • (e) Tume ya Huduma za Mahakama;
  • (f) Tume ya Ugavi wa Mapato;
  • (g) Tume ya Huduma za umma;
  • (h) Tume ya Ajira na Kuzawidi;
  • (i) Tume ya Kuwaajiri Walimu; na
  • (j) Tume ya Huduma za Polisi za Kitaifa.

(3) Afisi huru ni-

  • (a) Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu; na
  • (b) Msimamizi wa Bajeti.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-15/kifungu-248/utekelezaji-wa-sura/