(1) Malengo ya Tume na afisi huru ni–
- (a) kulinda mamlaka ya watu;
- (b) kuhakikisha kwamba idara zote za serikali zinazingatia kanuni na maadili ya kidemokrasia; na
- (c) kuendeleza mfumo wa kikatiba.
(2) Tume na wanaoshikilia nyadhifa za afisi huru–
- (a) wako chini ya Katiba hii pamoja na sheria; na
- (b) wako huru na hawawezi kuelekezwa au kudhibitiwa na mtu yeyote au idara.
(3) Bunge litatenga fedha za kutosha kuwezesha kila tume na afisi huru kutekeleza majukumu yake na bajeti ya kila tume na afisi huru itakuwa kando.