(1) Kila mtu ana haki ya kuwasilisha kesi mahakamani, akidai kuwa Katiba hii imekiukwa, au inatishiwa na kukiukwa.
(2) Pamoja na mtu anayefanya hivyo kwa maslahi yake mwenyewe kesi inaweza kuwasilishwa mahakamani kulingana na ibara ya (1) na–
- (a) mtu anayewasilisha kwa niaba ya mwingine ambaye hawezi kufanya hivyo yeye binafsi;
- (b ) mtu anayewasilisha kama mwanachama wa, au kwa maslahi ya, kundi au makundi ya watu;
- (c) mtu anayewasilisha kwa niaba ya maslahi ya umma; au
- (d) chama kinachowasilisha kwa maslahi ya mmoja au zaidi ya wanachama wake.