(1) Maadili ya kitaifa, kanuni na malengo yaliyo katika Sura hii yatazingatiwa na idara mbalimbali za Serikali, watumishi wa umma na watu wote wanapo–-
- (a) tekeleza au kufasiri Katiba hii;
- (b) tumia, tekeleza au kufasiri sheria yoyote; au
- (c) tunga, au kutekeleza maamuzi kuhusu sera ya kitaifa.
(2) Maadili ya kanuni za uongozi ni pamoja na-–
- (a) uzalendo, umoja wa kitaifa, kushirikiana na ugatuzi wa mamlaka, utawala wa sheria, demokrasia na kushiriki kwa watu;
- (b) heshima ya binadamu, usawa, haki za jamii, kushirikishwa, haki za binadamu, kutobagua na kulindwa kwa makundi yaliyotengwa.
- (c) utawala mwema, uadilifu, uwazi na uwajibikaji; na
- (d) maendeleo endelevu.