Ruka hadi Yaliyomo

(1) Lugha ya taifa ya Jamhuri ni Kiswahili.

(2) Lugha rasmi za Jamhuri ya Kenya ni Kiswahili na Kiingereza.

(3) Serikali–

  • (a) Itakuza na kulinda lugha tofauti za wananchi wa Kenya; na
  • (b) Italinda na itastawisha matumizi ya lugha za kiasili, Lugha Ishara ya Kenya, Breli na njia nyingine za mawasiliano na teknolojia zinazoweza kufikiwa na watu wenye ulemavu.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-2/kifungu-7/lugha/