(1) Alama za kitaifa za Jamhuri ni-–
- (a) bendera ya taifa;
- (b) wimbo wa taifa;
- (c ) nembo ya taifa; na
- (d) muhuri wa Serikali.
(2) Alama za kitaifa ni kama zilivyotajwa katika Mpangilio wa Pili.
(3) Siku kuu za kitaifa ni –
- (a) Siku kuu ya Madaraka, kuadhimishwa Juni 1;
- (b) Siku kuu ya Mashujaa, kuadhimishwa Oktoba 20; na
- (c) Siku kuu ya Jamhuri, kuadhimishwa Disemba 12.
(4) Siku kuu ya kitaifa itakuwa siku ya mapumziko kote nchini.
(5) Bunge linaweza, kupitia kwa sheria, kuamua ni siku gani itakuwa ya kitaifa na kuelekeza maadhimisho yake kama siku ya mapumziko.