Ruka hadi Yaliyomo

(1) Kila raia–

  • (a) anastahiki kupata haki, fursa, na faida kwa mujibu wa Katiba hii; na
  • (b) ana haki ya kupata hati ya usafiri ya Kenya na hati yoyote ya usajiliwa au utambulisho unaotolewa na Serikali kwa raia wake.

(2) Hati ya usafiri au hati nyingine ya usajili au utambulisho iliyotajwa katika ibara ya (1) inaweza kunyimwa mtu, kusimamishwa kwa muda au kupokonywa mtu kwa mujibu wa Sheria ya Bunge ambayo inatosheleza kigezo kilichotajwa katika Kifungu cha 24.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-3/kifungu-12/haki-za-raia/