(1) Kila mtu ni raia wa Kenya iwapo, wakati wa siku ya kuzaliwa kwake, iwe amezaliwa nchini Kenya au la, bora tu ikiwa mama au baba yake ni raia.
(2) Ibara ya (1) itatumika sawa kwa mtu ambaye alizaliwa kabla ya siku ya kuanza kutumika kwa Katiba hii, iwe amezaliwa nchini au la, ikiwa mama au baba yake ni, au alikuwa raia.
(3) Bunge linaweza kutunga sheria kuwekea mipaka athari za ibara ya (1) na (2) kwa raia wa Kenya ambao wamezaliwa nje ya Kenya.
(4) Mtoto anayepatikana nchini Kenya ambaye anaonekana kuwa na umri wa chini ya miaka minane, na ambaye uraia wake haujulikani na pia wazazi hawajulikani, atachukuliwa kuwa raia kwa kuzaliwa.
(5) Mtu ambaye ni raia wa Kenya kwa kuzaliwa na ambaye amekoma kuwa raia kwa sababu ya kupata uraia wa nchi nyingine ana haki, kwa kutuma maombi, kurejeshewa uraia wa Kenya.