Ruka hadi Yaliyomo

(1) Mahakama Kuu ina mamlaka kwa mujibu wa Kifungu cha 165 kusikiliza upya na kuamua kesi inayohusu kunyimwa, kukiukwa, kuvunjwa au kutishiwa kwa haki au uhuru wa kimsingi katika Sheria ya Haki.

(2) Bunge litatunga sheria kutoa uwezo wa kiasili kwa mahakama ya chini katika kusikizwa upya na kuamuliwa kwa kesi dhidi ya kunyimwa, kuvunjwa kukiukwa kwa Sheria ya Haki.

(3) Katika kesi yoyote inayoletwa mbele yake chini ya Kifungu cha 22, mahakama inaweza kutoa usaidizi, ukiwemo-

  • (a) kukiri haki;
  • (b) agizo la kusimamisha kesi;
  • (c) amri ya uhifadhi;
  • (d) kutangaza kutofaa kwa sheria yoyote inayonyima, kuvunja, kuingilia na kutishia Sheria ya Haki na isiyokubalika kwa misingi ya Kifungu cha 24;
  • (e) amri ya kufidiwa; na
  • (f) amri ya marekebisho ya kisheria
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-4/sehemu-1/kifungu-23/mamlaka-ya-mahakama/