Kila mtu ana haki ya uhuru na usalama wake unaohusisha haki ya–
- (a) kutonyimwa uhuru kiholela bila sababu;
- (b) kutozuiliwa bila kushtakiwa mahakamani, isipokuwa wakati wa hali ya hatari ambapo kifungo cha aina hiyo kinaelezwa katika Kifungu cha 58;
- (c) kuwa huru dhidi ya aina zote za ghasia kutoka kwa umma au watu binafsi;
- (d) kutoteswa kwa njia yoyote ile, iwe ya kimwili au kiakili;
- (e) kutopewa adhabu ya viboko; au
- (f) kutotendewa au kupewa adhabu za kikatili, kudhalilisha au kushusha hadhi ya ubinadamu.