(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kuwa na msimamo, dini, mawazo, imani na maoni.
(2) Kila mtu ana haki, ama kibinafsi au na wengine katika jamii, kwa wazi au kifaragha, kufuata dini au imani yoyote kupitia ibada, matendo, mafundisho au maadhimisho, yakiwemo mazingatio ya siku za ibada.
(3) Mtu hatazuiwa kuingia ama kujiunga na taasisi yoyote, kunyimwa ajira au kufika mahali fulani au kufurahia haki yoyote kwa sababu ya imani yake ya kidini.
(4) Mtu hatalazimishwa kutenda au kujihusisha na kitendo chochote ambacho ni kinyume na imani ya dini yake.