(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kujieleza unaohusisha–
- (a) uhuru wa kutafuta, kupokea au kutoa habari au kauli;
- (b) uhuru wa ubunifu wa kisanii; na
- (c) uhuru wa kiakademia na utafiti wa kisayansi.
(2) Haki ya uhuru wa kujieleza haiambatani na–
- (a) propaganda ya vita;
- (b) uchochezi wa ghasia;
- (c) hotuba za chuki; au
- (d) utetezi wa chuki ambao–
- (i) unajumuisha uchochezi wa kikabila, kuwatusi wengine au uchochezi wa kusababisha maafa; au
- (ii) unaotokana na misingi yoyote ya ubaguzi iliyotajwa au kuonyeshwa katika Kifungu cha 27 (4).
(3) katika kutekeleza uhuru wa kujieleza, kila mtu ataheshimu haki na hadhi ya watu wengine.