Ruka hadi Yaliyomo

(1) Kila mwananchi ana haki ya kupata–

  • (a) habari ilizonazo Serikali; na
  • (b) habari zozote alizonazo mtu mwingine na zinazohitajika ili kutekeleza au kulinda haki yoyote au uhuru wowote wa kimsingi.

(2) Kila mtu ana haki ya kudai marekebisho au kubatilishwa kwa habari zozote za uongo au za kupotosha zinazomhusu mtu huyo.

(3) Serikali itachapisha na kutangaza taarifa yoyote inayoathiri taifa.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-4/sehemu-2/kifungu-35/upataji-habari/