Ruka hadi Yaliyomo

(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kutangamana ambayo inahusu hakimya kuanzisha, kujiunga na, au kushiriki katika majukumu ya mashirika.

(2) Mtu hatalazimishwa kujiunga na muungano wa aina yoyote.

(3) Sheria yoyote kuhusu usajili wa miungano ya makundi ya kijamii itahitaji kwamba–

  • (a) usajili huo hauwezi kuzuiwa au kuondolewa bila sababu maalum; na
  • (b) kutakuwa na haki ya kusikizwa kwa kesi hiyo kabla ya usajili huo kuvunjiliwa mbali.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-4/sehemu-2/kifungu-36/kutangamana/