Ruka hadi Yaliyomo

Kifungu 39. Uhuru wa Kutembea na Makaazi

(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kutembea.

(2) Kila mtu ana haki ya kuondoka nchini Kenya.

(3) Kila mwananchi ana haki ya kuingia, kubaki na kuishi kokote nchini Kenya.