(1) Kila mtu ana haki ya kanuni sawa za kikazi.
(2) Kila mfanyakazi ana haki ya–
- (a) kulipwa ipasavyo;
- (b) mazingira ya kufaa ya kufanyia kazi;
- (c) kuunda, kujiunga au kushiriki katika shughuli na mipango ya vyama vya wafanyakazi; na
- (d) kugoma.
(3) Kila mwajiri ana haki ya–
- (a) kuunda au kujiunga na vyama vya waajiri; na
- (b) kushiriki katika shughuli na mipango ya vyama vya waajiri.
(4) Kila chama cha wafanyakazi na vyama vya waajiri vina haki ya–
- (a) kuamua usimamizi wake, mipango na shughuli zake;
- (b) kupanga; na
- (c) kuunda na kujiunga na shirikisho.
(5) Kila chama cha wafanyakazi, muungano wa wajiri na mwajiri wana haki ya kushiriki katika maafikiano ya pamoja.