(1) Kila mtu ana haki ya–
- (a) kupata kiwango cha juu kabisa kinachowezekana cha afya, kinachohusu haki ya huduma za malezi ya kiafya ikiwa ni pamoja na malezi ya afya ya uzazi;
- (b) kupata makao ya kuridhisha, na viwango vinavyostahili vya usafi
- (c) kutokuwa na njaa, na kupata chakula cha kutosha na kinachostahili;
- (d) kupata maji safi na salama na ya kutosha;
- (e) usalama wa kijamii ; na
- (f) elimu.
(2) Mtu hatanyimwa matibabu ya dharura.
(3) Serikali itatoa ulinzi wa kijamii unaofaa kwa wale ambao hawawezi kujisimamia wao wenyewe na jamii zao.