(1) Kila mtu ana haki ya kutumia lugha na kushiriki katika maisha ya kitamaduni ya chaguo lake.
(2) Mtu anayetoka katika jamii ya utamaduni au lugha fulani ana haki, pamoja na wanajamii wenzake–
- (a) kufurahia utamaduni wake na kutumia lugha yake; au
- (b) kuunda, kujiunga na kudumisha vyama vya kitamaduni na kilugha na miungano mingine ya raia katika jamii.
(3) Mtu hatamlazimisha mwingine kufanya, kuzingatia au kupitia mila zozote za kitamaduni.