(1) Watumiaji wa bidhaa na huduma wana haki ya–
- (a) kupata bidhaa na huduma za ubora wa kukubalika;
- (b) habari zenye manufaa kwao ili waweze kupata faida kamili kutokana na huduma na bidhaa hizo;
- (c) kulindwa afya yao, usalama wao, na maslahi yao ya kiuchumi; na
- (d) kufidiwa kwa hasara au matatizo yatakayotokana na kasoro ya bidhaa au huduma hizo.
(2) Bunge litatunga sheria ya kuhakikisha ulinzi wa watumiaji na wa matangazo huru, kweli na ya kufaa.
(3) Kifungu hiki kinahusu bidhaa na huduma zitakazotolewa na mashirika ya umma au watu binafsi.