(1) Watu wenye ulemavu wana haki ya–
- (a) kuheshimiwa na kupewa heshima ya binadamu ikiwemo, kushughulikiwa, kuzungumziwa na kutajwa, kwa njia isiyowadunisha au kuwadhalilisha;
- (b) kupata elimu katika taasisi za elimu na vifaa vya watu wenye ulemavu vilivyofungamanishwa na jamii kwa minajili ya maslahi yao;
- (c) kufikia ipasavyo sehemu zote zinazofikwa na umma, usafiri wa umma na habari na mawasiliano;
- (d) kutumia lugha ya ishara, Breli, na njia nyingine mwafaka za mawasiliano; na
- (e) kupata nyenzo na vifaa vinavyoweza kuwasaidia kukabiliana na matatizo ya ulemavu huo;
(2) Serikali itahakikisha kuendelea kwa utekelezaji wa kanuni kwamba, angalau asilimia tano ya maafisa katika mashirika, wanaochaguliwa au kuteuliwa, ni watu wenye ulemavu.