Ruka hadi Yaliyomo

Serikali itachukua hatua, ikiwemo miradi ya vitendo sawazishi, kuhakikisha kwamba vijana–

  • (a) wanapata elimu na mafunzo yanayofaa;
  • (b) wana fursa ya kujumuika, kuwakilishwa na kushiriki katika nyanja za kisiasa, kijamii kiuchumi na nyanja nyingine za maisha;
  • (c) wanapata kazi; na
  • (d) kulindwa dhidi ya tamaduni zinazodhuru na kunyanyasa.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-4/sehemu-3/kifungu-55/vijana/