Ruka hadi Yaliyomo

Serikali itatekeleza mipango inayonuia kuhakikisha kuwa makundi yaliyotengwa na kubaguliwa–

  • (a) yanashiriki na kuwakilishwa katika uongozi na nyanja zote za maisha;
  • (b) yanapewa nafasi maalum katika nyanja za elimu na uchumi;
  • (c) yanapewa fursa maalum ya kuajiriwa;
  • (d) yanakuza tamaduni zao, lugha na kaida zao; na
  • (e) yanapata maji , huduma za afya na miundombinu ya usafiri;
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-4/sehemu-3/kifungu-56/waliotengwa-na-kubaguliwa/