Bunge–
- (a) litarekebisha, kuunganisha na kusawazisha sheria zilizopo kuhusu ardhi;
- (b) litarekebisha sheria za kisekta kuhusu matumizi ya ardhi kwa mujibu wa kanuni zilizotajwa katika Kifungu cha 60 (1);
- (c) litatunga sheria–
- (i) kushauri kuhusu kiwango cha juu na cha chini cha ekari za ardhi ya kumilikiwa baada ya kuzingatia ardhi ya kibinafsi;
- (ii) kudhibiti njia ambazo ardhi yoyote inaweza kubadilishwa kutoka kwenye ngazi moja hadi nyingine;
- (iii) kudhibiti utambuaji na uhifadhi wa mali ya kindoa na hasa boma la kindoa wakati wa ndoa na wakati wa uvunjwaji wa ndoa hiyo;
- (iv) kulinda, kuhifadhi na kutoa nafasi ya kupatikana kwa ardhi yote ya umma;
- (v) kuwezesha kuchunguzwa upya kwa nafasi ya ardhi ya umma ili kuimarisha mali au uhalali wake;
- (vi) kuwalinda wategemezi wa jamaa za wafu na haja ya kupata ardhi yakiwemo maslahi ya mume na mke wanaoishi katika ardhi;
- (vii) kutoa nafasi kwa suala jingine lolote linalohitajika katika kuendeleza masharti ya Sura hii.