Ruka hadi Yaliyomo

(1) Iwapo mtu anadai kuwa haki ya kupata mazingira safi na yenye afya inayotambuliwa na kulindwa chini ya Kifungu cha 42 imekiukwa, inakiukwa au inaelekea kukiukwa, kunyimwa, kuvunjwa au kutishiwa, mtu huyo anaweza kuwasilisha kesi mahakamani ili asikilizwe mbali na hatua nyingine za kisheria zitakazoshughulikia suala hilo.

(2) Kutokana na ombi chini ya ibara ya (1), mahakama inaweza kutoa amri au maelekezo yanayostahili–

  • (a) kuzuia, kukomesha au kuachisha tendo au kosa lolote hatari kwa mazingira;
  • (b) kumshurutisha afisa yeyote wa umma kuchukua hatua ya kuzuia au kukomesha tendo au kosa lolote hatari kwa mazingira; ama
  • (c) kutoa fidia kwa mwathiriwa yeyote anayeathirika kutokana na ukiukaji wowote wa haki ya kupata mazingira safi na salama kiafya.

(3) Kwa madhumuni ya Kifungu hiki, haitakuwa lazima kwa anayetoa maombi kuonyesha kwamba mtu amepata hasara au kujeruhiwa

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-5/sehemu-2/kifungu-70/haki-za-mazingira/