Ruka hadi Yaliyomo

(1) Mapatano yoyote yanaweza kuidhinishwa na Bunge iwapo-

  • (a) yanahusisha utoaji wa haki au makubaliano na, au kwa niaba ya mtu yeyote, ikiwemo Serikali ya taifa kwa mtu mwingine, ya kutumia maliasili yoyote iliyo nchini Kenya; na
  • (b) yataafikiwa siku ya kuanza kutumia Katiba hii au baadaye.

(2) Kupitia utungaji wa sheria, Bunge litatoa viwango vya maafikiano yatakayoidhinishwa chini ya ibara ya (1).

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-5/sehemu-2/kifungu-71/maliasili/