Ruka hadi Yaliyomo

Bunge litatunga sheria–

  • (a) kubuni taratibu na mikakati ya kutekeleza sura hii kwa njia ifaayo;
  • (b) kupendekeza adhabu zaidi ya zile zinazotajwa katika Kifungu cha 75, ambazo zinaweza kuamriwa kwa sababu ya kutofuata maagizo ya Sura hii;
  • (c) kusaidia katika utekelezaji wa Sura hii pakiwa na marekebisho yanayofaa kwa maafisa wa umma; na
  • (d) kuunda masharti mengine yoyote katika kuhakikisha udumishaji wa kanuni za uongozi na uadilifu ambayo yametajwa katika Sura hii, na utekelezaji wa masharti ya Sura hii.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-6/kifungu-80/sheria-kuhusu-uongozi/