Mfumo wa uchaguzi utazingatia kanuni zifuatazo–
- (a) uhuru wa raia wa kutekeleza haki zao za kisiasa chini ya Ibara ya 38;
- (b) sio zaidi ya thuluthi mbili ya wanachama wa mashirika ya umma yatakayoshiriki uchaguzi wa wanachama watakuwa ya jinsia sawa;
- (c) uwakilishi wenye usawa wa watu walio na ulemavu;
- (d) haki ya kupiga kura kwa wote katika misingi ya haki ya uwakilishwaji na usawa wa kura; na
- (e) chaguzi za haki na usawa, ambazo ni–
- (i) za kura ya siri;
- (ii) huru na zisizo na ghasia, vitisho, ushawishi usiofaa, au ufisadi;
- (iii) zinazoendeshwa na halmashauri huru;
- (iv) wazi; na
- (v) zinazofanywa kwa njia zisizopendelea upande wowote, katikati, bora, kamilifu na zilizo na uwajibikaji.