Ruka hadi Yaliyomo

(1) Mtu anastahili kusajiliwa kama mpiga kura katika chaguzi au kura za maamuzi kama mtu huyo–

  • (a) ni raia mtu mzima;
  • (b) hajatangazwa kuwa na akili punguwani; na
  • (c) hajapatikana na hatia ya uchaguzi katika kipindi cha mitano iliyotangulia.

(2) Raia anayestahili kusajiliwa kama mpigakura atasajiliwa kwenye kituo kimoja tu cha usajili wa kupigia kura.

(3) Mipango ya kiusimamizi ya usajili wa wapiga kura na uendeshaji wa chaguzi, itapangwa ili kurahisisha, na haitamnyima raia yeyote anayestahili haki ya kupiga kura au kugombea uchaguzi.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-7/sehemu-1/kifungu-83/kusajiliwa/