Mtu yeyote anastahili kusimama kama mgombea uchaguzi wa kujitegemea, ikiwa mtu huyo–
- (a) si mwanachama wa chama cha kisiasa kilichosajiliwa na hajakuwa mwanachama kwa angalau kwa kipindi cha miezi mitatu kabla ya tarehe ya uchaguzi; na
- (b) anatimiza masharti ya–
- (i) Kifungu cha 99 (1) (c) (i) au (ii), kwa mgombeaji wa uchaguzi wa Baraza la Kitaifa au Seneti, mtawalia; au
- (ii) Kifungu cha sheria cha 193 (1) (c) (ii), kwa wa uchaguzi wa bunge la kaunti.