Ruka hadi Yaliyomo

(1) Bunge litatunga sheria ya kubuniwa kwa mifumo ya kusuluhishwa kwa haraka mizozo ya uchaguzi.

(2) Malalamiko kuhusu uchaguzi, isipokuwa uchaguzi wa urais, yatawasilishwa katika kipindi cha siku ishirini na nane baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka.

(3) Kukabidhiwa kwa mashtaka hayo kunaweza kuwa kwa moja kwa moja au kupitia kwa tangazo katika gazeti linalosambazwa kote nchini.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-7/sehemu-1/kifungu-87/mizozo-ya-uchaguzi/