Ruka hadi Yaliyomo

Bunge litatunga sheria ambayo itatoa–

  • (a) nafasi sawa ya kutengewa muda katika vyombo vya habari, vinavyomilikiwa na Serikali au aina ya vyombo vinginevyo vya utangazaji, kwa vyama vya kisiasa wakati wowote au wakati wa kampeni za uchaguzi; na
  • (b) udhibiti wa uhuru wa kutangaza ili kuhakikisha kampeni zilizo na haki wakati wa uchaguzi;
  • (c) udhibiti wa vyama vya kisiasa;
  • (d) majukumu na utendakazi wa vyama vya kisiasa;
  • (e) usajili na usimamizi wa vyama vya kisiasa;
  • (f) uundwaji na uongozi wa hazina ya vyama vya kisiasa;
  • (g) akaunti na ukaguzi wa hesabu za vyama vya kisiasa;
  • (h) masharti kuhusu matumizi ya rasilimali ya umma ili kuendeleza maslahi ya vyama vya kisiasa; na
  • (i) masuala mengine muhimu ya kuongoza vyama vya kisiasa.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-7/sehemu-3/kifungu-92/sheria-ya-vyama/