Ruka hadi Yaliyomo

(1) Seneti inawakilisha kaunti na inatumika kulinda maslahi ya kaunti na serikali zake.

(2) Seneti inashiriki katika jukumu la Bunge la uundaji wa sheria kwa kuamua, kujadiliana, kuidhinisha miswada inayohusu kaunti kama ilivyo katika Kifungu cha 109 hadi 113.

(3) Seneti ndio huamua ugavi wa mapato ya kitaifa miongoni mwa kaunti kama ilivyo katika Kifungu cha 217, na kutekeleza usimamizi jumla wa mapato ya kitaifa iliyotengewa kwa serikali za kaunti.

(4) Seneti inashiriki katika usimamizi wa maafisa wa Serikali na kutathmini na kutoa maamuzi kuhusu hoja ya kumuondoa Rais au Naibu wa rais kutoka kwenye wadhifa wake kwa mujibu wa Kifungu cha 145.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-8/sehemu-1/kifungu-96/jukumu-la-seneti/