Uchaguzi mkuu wa wabunge utafanyika Jumanne ya pili ya mwezi wa Agosti katika kila mwaka wa tano.
(2) panapotokea nafasi katika afisi ya mbunge wa Baraza la Kitaifa, lililotajwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (c), au katika Seneti chini ya Kifungu cha 98 (1) (b), (c) ama (d), Spika mhusika, katika kipindi cha siku ishirini na moja za kutokea nafasi hiyo ya kazi, atatoa notisi kwa maandishi kuhusu nafasi hiyo ya kazi kwa–
- (a) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka; na
- (b) chama cha kisiasa ambacho kupitia kwa orodha yake ya chama ndipo mwanachama huyo alipokuwa amechaguliwa au kuteuliwa.
(3) Nafasi hiyo iliyotajwa katika Ibara ya (2) kwa, kuambatana na Ibara ya (5), itajazwa kwa namna iliyoagizwa na Sheria ya Bunge ndani ya muda wa siku ishirini na moja baada ya kutangazwa na Spika mhusika.
(4) Panapotokea nafasi ya kazi katika afisi ya mwanachama wa Baraza la Kitaifa aliyechaguliwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (a) au (b), au wa Seneti aliyechaguliwa chini ya Kifungu cha 98 (1) (a)–
- (a) Spika mhusika, kwa muda wa siku ishirini na moja baada ya kutokea kwa nafasi hii , atatoa notisi kuhusu nafasi hii kwa kuiandikia Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka; na
- (b) uchaguzi mdogo utafanyika katika muda wa siku baada ya kutokea kwa nafasi hiyo ya kazi, kuambatana na ibara ya (5).
(5) Nafasi iliyotajwa katika ibara ya (4) haitajazwa katika kipindi cha miezi mitatu inayotangulia uchaguzi mkuu.