Ruka hadi Yaliyomo

(1) Muhula wa kila Bunge humalizika mnamo tarehe ya uchaguzi mkuu unaofuata.

(2) Wakati Kenya iko kwenye vita, mara kwa mara Bunge, kwa maamuzi yalioungwa mkono na angalau wabunge wasiopungua thuluthi mbili ya wabunge wote katika kila kitengo cha bunge, linaweza kuongeza kipindi cha Bunge kwa muda usiozidi miezi sita kwa wakati huo.

(3) muhula wa bunge hautaongezwa chini ya ibara ya (2) kwa jumla ya zaidi ya miezi kumi na miwili.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-8/sehemu-2/kifungu-102/muhula-wa-bunge/