Ruka hadi Yaliyomo

(1) Wapiga kura chini ya Vifungu vya 97 na 98, wana haki ya kumuondoa mamlakani mbunge waliyemchagua ili kuwakilisha eneobunge kabla ya kukamilika kwa kipindi cha Bunge.

(2) Bunge litatunga sheria inayoorodhesha sababu za kufaa na taratibu zitakazofuatwa za kumuondoa mbunge mamlakani.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-8/sehemu-2/kifungu-104/kumwondoa-mbunge/