Ruka hadi Yaliyomo

(1) Isipokuwa wakati mtu amepigwa marufuku katika ugombeaji chini ya Ibara ya (2), mtu anaweza kuchaguliwa kama mbunge iwapo mtu huyo–

  • (a) amesajiliwa kama mpigakura;
  • (b) anaafiki kiwango chochote cha kielimu, kimaadili na ana uadilifu kama inavyoagizwa kwenye Katiba hii au na Sheria ya Bunge; na
  • (c ) ameteuliwa na chama cha kisiasa au mgombeaji wa kujitegemea anayedhaminiwa–
    • (i) na angalau wapigakura elfu moja waliosajiliwa katika eneobunge katika uchaguzi wa Baraza la Kitaifa; na
    • (ii) na angalau wapigakura elfu mbili waliosajiliwa katika kaunti kwa uchaguzi wa Seneti.

(2) Mtu hastahili kuchaguliwa kama mbunge ikiwa mtu huyo–

  • (a) anashikilia jukumu lolote la Serikali au afisi mwingine wa umma, licha ya kuwa Mbunge;
  • (b) amekuwa, katika kipindi cha miaka mitano inanayotangulia taratibu za uchaguzi, ameshawahi kushikilia afisi kama mwanachama wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka;
  • (c) hakuwa raia wa Kenya kwa angalau miaka kumi inayotangulia tarehe ya uchaguzi;
  • (d) ni mwanachama wa Baraza la Kaunti;
  • (e) hana akili timamu;
  • (f) mufilisi ;
  • (g) anakabiliwa na hukumu ya kifungo cha miezi sita gerezani, kuanzia siku ya kujiandikisha kama mgombeaji, au katika tarehe ya uchaguzi; au
  • (h) amepatikana, kwa mujibu wa sheria yoyote, kutumia vibaya afisi ya Serikali au ya umma ama kwa njia yoyote alikiuka kanuni za Sura ya Sita.

(3) Mtu hazuiliwi chini ya ibara ya (2) isipokuwa tu pale ambapo uwezekano wote wa rufaa au kubadilishwa kwa kifungo kinachofaa ama pamekosekana maamuzi mengine.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-8/sehemu-2/kifungu-99/sifa-za-mbunge/