Ruka hadi Yaliyomo

(1) Kutakuwa na–

  • (a) Spika wa kila kitengo cha Bunge, atakayechaguliwa na kitengo hicho kulingana na Kanuni za Kuendesha Bunge, kutoka miongoni mwa watu walio na sifa zinazostahili kuchaguliwa kama wabunge na ambao si wabunge; na
  • (b) Naibu Spika wa kila Bunge, atakayechaguliwa na Bunge hilo kwa mujibu wa Kanuni za Kuendesha Bunge, kutoka miongoni mwa wabunge.

(2) Afisi ya Spika au Naibu wa Spika itakuwa wazi–

  • (a) wakati Bunge litakapokutana kwa mara ya kwanzabaada ya uchaguzi;
  • (b) iwapo anayeshikilia afisi, kama mwanachama wa Bunge husika, anaondoka afisini chini ya Kifungu cha 103;
  • (c) iwapo Bunge husika linaamua kwa uamuzi ulioungwa mkono na angalau wabunge wasiopungua thuluthi mbili; ama
  • (d) iwapo anayeshikilia afisi hiyo atajiuzulu kutoka kwa afisi hiyo kwa kuandika barua kwa Bunge husika.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-8/sehemu-3/kifungu-106/spika-wa-bunge/