Ruka hadi Yaliyomo

(1) Kutakuwa na Kiongozi wa chama kilicho na idadi kubwa ya wabunge na kiongozi wa chama cha walio wachache Bungeni.

(2) Kiongozi wa chama kilicho na wabunge wengi ndiye atakayekuwa kiongozi katika Baraza la Kitaifa la chama kilicho na idadi kubwa ya wabunge au muungano wa vyama;

(3) Kiongozi wa chama cha walio wachache ni kiongozi katika Baraza la Kitaifa la chama kilicho cha pili kwa idadi ya wabunge au muungano wa vyama;

(4) Mpangilio ufuatao wa kupewa umuhimu wa kwanza utafuatwa katika Baraza la Kitaifa–

  • (a) Spika wa Baraza la Kitaifa;
  • (b) Kiogozi wa chama cha wabunge walio wengi;
  • (c) Kiongozi wa chama cha wabunge walio wachache.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-8/sehemu-3/kifungu-108/viongozi-wa-vyama/