Ruka hadi Yaliyomo

(1) Mswada wa fedha hauwezi kushughulikia suala jingine lolote isipokuwa tu lile ambalo limeorodheshwa katika fasiri ya ‘Mswada wa fedha’ kwenye ibara ya (3).

(2) Iwapo, kwa maoni ya Spika wa Baraza la Kitaifa, mjadala unatoa vifungu kwa suala lililotajwa katika fasiri ya Mswada wa fedha, Bunge linaweza kuendelea tu kwa mujibu wa mapendekezo ya kamati husika ya Bunge baada ya kutilia maanani maoni ya Waziri anayehusika na fedha.

(3) Katika Katiba hii, ‘Mswada wa fedha’ unamaanisha , Mswada, tofauti na Mswada uliotajwa katika Kifungu cha 218 kilicho na masharti yanayoshughulikia–

  • (a) ushuru;
  • (b) kutoza malipo kwa hazina ya umma au kubadili au kuondolewa kwa mojawapo wa malipo hayo;
  • (c ) kugawa, kupokea, kutunza, kuwekeza au kutoa pesa za umma;
  • (d) kudhamini mkopo wowote au ulipwaji wake; ama
  • (e) masuala mengineyo yanayotokana na masuala hayo.

(4) Katika ibara ya (3), “ushuru”, “fedha za umma”, na “mkopo”, hazijumuishi ushuru wowote, fedha za umma au mkopo uliopatwa na kaunti.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-8/sehemu-4/kifungu-114/miswada-ya-fedha/