Ruka hadi Yaliyomo

(1) Ila tu, kulingana na maagizo katika Katiba hii, Suala lolote litakalopendekezwa kuamuliwa katika mojawapo wa Bunge, litaamuliwa kwa kupigiwa kura na wingi wa wabunge waliopo.

(2) Katika swali linalopendekezwa kuamuliwa katika mojawapo wa Bunge–

  • (a) Spika hatapiga kura; na
  • (b) Iwapo kura zitakuwa sawa pande zote, swali hilo litakuwa limeshindwa.

(3) Mbunge hatapigia kura suala ambalo yeye mwenyewe ana maslahi ya kifedha.

(4) Katika kujumlisha idadi ya wabunge kwenye Bunge kwa kusudi lolote la kupiga kura katika Bunge hilo, Spika wa bunge hilo hatahesabiwa.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-8/sehemu-5/kifungu-122/kupiga-kura-bungeni/