(1) Kila Bunge linaweza kubuni kamati, na kuweka kanuni za kuendesha Bunge ili kusimamia shughuli zake ikiwa ni pamoja na shughuli za kamati zake.
(2) Bunge linaweza kubuni kamati za pamoja zinazojumuisha wabunge kutoka Mabunge yote mawili na kwa pamoja kudhibiti utaratibu wa kamati hizo.
(3) Shughuli za kila mojawapo ya Mabunge hayo hazitaharamishwa eti kwa sababu ya–
- (a) nafasi katika uanachama wake; au
- (b) kuwepo au kushiriki kwa mtu yeyote asiyepaswa kuwepo au kushiriki katika shughuli za bunge hilo.
(4) Wakati Bunge litakaposhughulikia kuhusu uteuzi wowote pale ambapo idhini inahitajika kama inavyotakikana na Katiba hii au Sheria ya Bunge–
- (a) uteuzi huo utashughulikiwa na kamati husika ya Bunge;
- (b) mapendekezo ya kamati yatawasilishwa Bungeni ili kuidhinishwa; na
- (c) shughuli za kamati na za Bunge zitakuwa wazi kwa umma.