(1) Rais–
- (a) ndiye Kiongozi wa Taifa na Serikali;
- (b) anatekeleza mamlaka makuu ya Jamhuri kwa usaidizi wa Naibu wa Rais na Mawaziri;
- (c) ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Kenya;
- (d) ndiye mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa la Usalama
- (e) ni ishara ya umoja wa kitaifa.
(2) Rais–
- (a) ataiheshimu, kuifuata na kuilinda Katiba;
- (b) ataulinda uhuru wa Jamhuri ya Kenya.
- (c) atakuza na kudumisha umoja wa taifa.
- (d) atakuza heshima ya uanuwai wa watu wa Kenya; na
- (e) kuhakikisha ulinzi wa uhuru na haki za kimsingi za raia na utawala wa sheria.
(3) Rais hatasimamia afisi nyingine yoyote ya Serikali au ya umma.