(1) Kwa ombi la mtu yeyote, Rais anaweza kutekeleza mamlaka yake ya msamaha kwa mujibu wa ushauri kutoka kwa Kamati ya Ushauri iliyoundwa katika Kifungu cha (2) , kwa–
- (a) Kumsamehe kabisa au kwa masharti mtu ambaye amepatikana na hatia;
- (b) kuahirisha utekelezaji wa adhabu kwa muda uliowekwa au kwa muda usiojulikana;
- (c) Kubadili adhabu isiwe kali; au
- (d) Kusamehe sehemu ya adhabu au adhabu yote.
(2) Kutakuwepo na Kamati ya Ushauri kuhusu Mamlaka ya Msamaha wa Rais, itakayowahusisha–
- (a) Mwanasheria Mkuu;
- (b) Waziri anayehusika na Huduma za Urekebishaji; na
- (c) Angalau watu wengine watano,na wasiwe watu walio kwenye huduma ya umma au afisi za Serikali kama inavyoidhinishwa na Sheria ya Bunge.
(3) Bunge litatunga Sheria ili kubainisha–
- (a) hatamu ya wanachama wa Kamati ya Ushauri;
- (b) Taratibu za Kamati ya Ushauri; na
- (c) Kigezo ambacho kitatumiwa na Kamati ya Ushauri katika kuunda ushauri wake.
(4) Kamati ya Ushauri inaweza kutilia maanani maoni ya waathiriwa wa hatia kuhusu yale inayompendekezea Rais.