Ruka hadi Yaliyomo

(1) Yeyote anayeshikilia afisi ya Rais au yule ambaye anayeidhinishwa kwa mujibu wa Katiba hii kutumia mamlaka ya Rais–

  • (a) Katika kipindi kinachoanzia mnamo tarehe ya kwanza kwenye uchaguzi wa Rais, na kukamilika wakati Rais mpya anapochukua hatamu za afisi; au
  • (b) wakati Rais hayupo au, hawezi kutekeleza mamlaka yake au wakati mwingine kama ilivyoelekezwa katika kifungu cha 147 (3), hawezi kutekeleza mamlaka ya Rais yaliyotajwa katika ibara ya ya (2).

(2) Mamlaka hayo yaliyotajwa katika ibara ya (1) ni–

  • (a) kuteua na kuwaandika kazi majaji wa mahakama yenye mamlaka makuu;
  • (b) kuteua na kuandika kazi afisa yeyote wa umma ambaye Katiba au sheria hii inamhitaji Rais kumteua;
  • (c) kuwaandika kazi au kuwateua au kuwaachiza kazi mawaziri na maafisa wengine wa umma au wa Serikali;
  • (d) Kuandika kazi au kuteu au kuwaachisha kazi mabalozi au wawakilishi wa mabalozi, wanadiplomasia na wawakilishi wengine;
  • (e) Mamlaka ya msamaha wa Rais;
  • (f) Mamlaka ya kutuza heshima kwa jina la wananchi na Jamhuri.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-9/sehemu-2/kifungu-134/rais-wa-muda/