Ruka hadi Yaliyomo

(1) Rais atachaguliwa na wapigakura waliosajiliwa katika uchaguzi wa kitaifa utakaoendeshwa kwa mujibu wa Katiba hii na Sheria nyingine yoyote ya Bunge inayothibiti uchaguzi wa Rais.

(2) Uchaguzi wa Rais utafanyika–

  • (a) siku moja na ile ya uchaguzi mkuu wa Wabunge, ikiwa ni siku ya Jumanne ya pili ya mwezi Agosti ya kila mwaka wa tano; au
  • (b) katika hali ambazo zinatajwa kwenye Kifungu cha 146.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-9/sehemu-2/kifungu-136/uchaguzi-wa-rais/