(1) Mtu anastahili kupendekezwa kuwa mgombeaji wa urais iwapo–
- (a) ni raia kwa kuzaliwa;
- (b) amehitimu kugombea uchaguzi kama mbunge;
- (c) ameteuliwa na chama cha kisiasa au ni mgombeaji wa kujitegemea; na
- (d) ameteuliwa na wapigakura wasiopungua elfu mbili kutoka kwa kila kaunti zilizo nyingi.
(2) Mtu hastahili kuteuliwa kuwa mgombea urais iwapo–
- (a) anawajibikia taifa la kigeni;
- (b) ni afisa wa umma, anayeshikilia afisi yoyote ya Serikali au nyingine ya umma;
(3) Ibara ya (2) (b) haitatumika kwa–
- (a) Rais;
- (b) Naibu wa Rais; au
- (c) mbunge.