Ruka hadi Yaliyomo

(1) Mtu anaweza kuwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Juu kupinga uchaguzi wa Rais mteule katika muda wa siku saba baada ya tarehe ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais.

(2) Katika muda wa siku kumi na nne baada ya kuwasilishwa kwa malalamiko, Mahakama ya Juu itasikiza na kuamua kesi hiyo na uamuzi wake utakuwa wa mwisho.

(3) Iwapo Mahakama ya Juu itaamua kuwa uchaguzi wa Rais Mteule si halali, uchaguzi mpya utafanyika katika muda wa siku sitini baada ya uamuzi huo.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-9/sehemu-2/kifungu-140/uhalali-uchaguzi-urais/