(1) Kuapishwa kwa Rais Mteule kutafanyika wazi na mbele ya Jaji Mkuu na ikiwa Jaji Mkuu hayupo, basi mbele ya Naibu jaji mkuu.
(2) Rais Mteule ataapishwa Jumanne ya kwanza itakayofuata–
- (a) siku kumi na nne baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Urais isipokuwa matangazo hayo yawe yamepingwa kulingana na Kifungu cha 140; ama
- (b) siku ya saba kufuatia tarehe ambayo mahakama inatoa uamuzi na kutangaza kuwa uchaguzi ulikuwa halali, ikiwa malalamiko yoyote yalikuwa yamewasilishwa chini ya Kifungu cha 140.
(3) Rais Mteule anachukua hatamu za Urais kwa kuchukua na kutia sahihi kiapo cha uaminifu; na kiapo cha kutekeleza majukumu ya Urais kama ilivyoamriwa katika Ratiba ya Tatu.
(4) Bunge kupitia kwa sheria itatoa taratibu za sherehe za kuapishwa kwa Rais-mteule.