Ruka hadi Yaliyomo

(1) Afisi ya Rais itakuwa wazi iwapo mwenye afisi hiyo–

  • (a) amefariki;
  • (b) amejiuzulu kwa kumwandikia barua Spika wa Baraza la Kitaifa; au
  • (c) ama anawacha kuwa mamlakani kwa mujibu wa Kifungu cha 144 au 145, au masharti mengineyo ya Katiba hii.

(2) Pale ambapo nafasi ya kazi katika afisi ya Rais itakapotokea–

  • (a) Naibu wa rais atachukua mamlaka kama Rais kwa muda uliosalia wa kipindi cha Rais; au
  • (b) iwapo afisi ya Naibu wa rais ni wazi au Naibu wa rais hawezi kuchukua mamlaka ya Rais, Spika wa Baraza la Kitaifa atakuwa kaimu wa Rais na uchaguzi utafanyika katika muda wa siku sitini baada ya nafasi hiyo kutokea katika afisi ya Rais.

(3) Mtu anayechukua hatamu za uongozi kama Rais chini ya ibara ya (2) (a) au kufuatia uchaguzi unaoidhinishwa na ibara ya (2) (b), isipokuwa aondolewe mamlakani kwa mujibu wa Katiba hii, ataendelea na wadhifa huo mpaka uchaguzi mpya ufanyike na Rais aliyechaguliwa upya kuapishwa kufuatia uchaguzi unaofuatia kwa wakati uliowekwa wa kawaida ulio chini ya Kifungu cha 136 (1).

(4) Iwapo Naibu wa rais atachukua mamlaka kama Rais chini ya ibara ya (2) (a) au mtu anachaguliwa kwa afisi ya Rais chini ya Ibara ya (2) (b), Naibu wa rais au mtu yule aliyechaguliwa watachukuliwa kufuatia kifungu cha 142 (2) kuwa–

  • (a) wamehudumu kipindi kizima kama Rais, iwapo kufikia tarehe ya kuchukua mamlaka ya afisi, kumesalia muda wa zaidi ya miaka miwili unusu kabla ya tarehe ya uchaguzi utakaofuata ambao umeratibiwa chini ya Kifungu cha 136 (2) (a); au
  • (b) hawajahudumu kipindi kizima kama Rais kwa hali nyingine yoyote.
Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-9/sehemu-2/kifungu-146/nafasi-ya-kazi/