Ruka hadi Yaliyomo

(1) Kila mgombea uchaguzi wa Urais atateua mtu ambaye amehitimu kuchaguliwa kama Rais, kama mgombeaji wa Naibu wa Rais.

(2) Kwa sababu ya ibara ya (1), hakutakuwa na utaratibu tofauti wa uteuzi wa Naibu wa Rais na kifungu cha 137 (1) (d) hakitatumika kwa mgombeaji kiti cha Naibu wa Rais.

(3) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itatangaza yule ambaye ameteuliwa na Rais mteule kuwa ndiye Naibu wa Rais.

(4) Kuapishwa kwa Naibu wa Rais mteule kutafanyika mbele ya Jaji Mkuu au iwapo Jaji Mkuu hayupo, mbele ya Naibu wa Jaji Mkuu na wananchi.

(5) Naibu wa rais mteule atachukua hatamu za afisi kwa–

  • (a) Kula kiapo cha uaminifu; na
  • (b) Kiapo cha kutekeleza majukumu ya afisi kama ilivyoidhinishwa katika Ratiba ya Tatu.

(6) Kipindi cha afisi ya Naibu wa rais kitaanza kutumika kutoka siku ya kuapishwa kwa Naibu wa rais na kukoma–

  • (a) Wakati mtu atakayechaguliwa kama Rais anayefuata katika uchaguzi chini ya Kifungu cha (136) (2) (a) ataapishwa;
  • (b) Wakati Naibu wa rais atachukua mamlaka ya Rais; au
  • (c) Katika kijiuzulu , kifo au kuachishwa kazi kwa Naibu wa rais.

(7) Naibu wa rais anaweza, kwa wakati wowote, kujiuzulu kwa kumwandikiia barua Rais na kujiuzulu huku kutaanza kutekelezwa saa na tarehe iliyobainishwa katika barua hiyo au iwapo tarehe haijabainishwa, adhuhuri ya siku ya kupokelewa kwa barua hiyo.

(8) Hakuna mtu yoyote atakayehudumu kwa zaidi ya vipindi viwili kama Naibu wa rais.

Msimbo wa QR unaounganisha kwenye https://blog.afro.co.ke/sw/katiba/sura-9/sehemu-2/kifungu-148/kuapishwa-naibu-rais/